Tuesday, September 17, 2013


Tabia Zitakazokimbiza Wachumba
Posted by womanofchrist
Wasichana wengi wanalalamika mimi sijaolewa, akija mtu kunichumbia baada ya muda mfupi
anakata mawasiliano, hakuna anayetaka kunichumbia n.k. Ni kweli kuna wakati na kusudi kwa kila jambo lakini pia mara nyingine matendo yetu yanaweza kusababisha kupata na kukosa vitu fulani. Kuna tabia ambazo hufukuza na kukimbiza wakaka wanapotaka au wanapokuchumbia. Angalia kama unazo ufanye jitihada la sivyo unaweza mlaumu Mungu bure:
1. Mizaha mingi
Kuna mtu alisema ukipewa karama ya kuongea omba Mungu akupe na hekima, ni kweli kabisa. Haipendezi mtu kuwa unaongea hadi unapililiza na kuwafanya watu kujisikia vibaya. Maongezi yaliyojaa mizaha ya kupililiza kweli utamkimbiza potential husband. Kuwa na staha kwenye maongezi yako.
2. Kupenda kukosoa hadharani
Watu wanaokuzunguka wanakujua vizuri, ukiwa mtu wa kuwakosoa wengine hadharani hakika utaogopwa. Mtu anaongea katika lundo la watu akakosea kidogo wewe unamkosoa mbele za watu hiyo haifai, au mtu kavaa kakosea kupangilia wewe unamkosoa mbele za watu.
3. Kushurutisha
Ndio kwanza mmeanza mahusiano wewe unataka kujua tarehe ya harusi, unampangia marafiki zake na mahali pa kwenda, unapanga hadi makochi ya sebuleni kwenu yatakuwaje. Yani wewe ndiyo unakuwa na ratiba yake, usiende huku, nenda kule, njoo hapa, haaaa huyo atakuvumilia kwa muda tu. Akimpata kwenye kumheshimu hapo utaona anakata mawasiliano taratibu maana hakuna mwanaume anayetaka kushurutishwa.
4. Kuomba hela mara kwa mara
Leo hela ya saluni, kesho mtaji umekata, mara ada ya mdogo wako hajakaa sawa mama anaumwa dah.. sikatai kusaidiana ila usiwe ndio kila siku unataka kusaidiwa tena fedha. Unambeep akipiga unamwambia akutumie salio au Mpesa akituma unabeep tena akipiga unamwambia asante nimepata. Nakwambia hata kama anakupenda vipi ataazimia kukuacha kwa siri kama Yusufu.
Jichunguze na uchukue hatua, usije kumlaumu shetani kwa kosa lako mwenyewe..

0 Maoni:

Post a Comment

Tafuta  hapa

Kuhusu sisi

Karibu kwenye Blog hii, naamini hautatoka bure na wala hautajuta kuitembelea Blog hii. Karibu sana

Habari Maarufu

Blog Malimbali

All rights reserved by Mwafrikasili - Blog design by ARM's pRo. Powered by Blogger.

Tafsiri

Hati Miliki

© 2013 Mwafrikasili


Jiunge Nasi

Jisajilikwenye blog hii
Twitter
Facebook