Thursday, July 16, 2015


MSONGO WA MAWAZO (STRESS)
Msongo wa mawazo ni tatizo la kisaikolojia litokanalo na mwitikio wa mwili kutokana na jambo fulani linakukabili kwa wakati huo.Kwa kawaida mwili wa binadamu unapokutana na changamoto yoyote hujiandaa namna ya kukabiliana nayo au huunda mbinu ya kulikimbia tatizo/changamoto husika.Katika
mchakato huu wa kutafuta majibu mfumo wa mwili huachia homoni mablimbali ikiwemo Adrenaline ambayo hupelekea kuongezeka kwa kiwango cha sukari katika mzunguko wa damu hivyo kuathiri mfumo wa kinga mwilini. Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ushindwe kufanya shughuli zako za kila siku kwa ufanisi au kupata magonjwa kama vile Mgandamizo mkubwa wa damu (BP) au kuongezeka kwa glokos mwilini
Msongo wa mawazo huathiri pia mfumo wa akili ya binadamu hivyo hupunguza uwezo wa kufikiri,hupunguza uwezo wa kukumbuka na mpangilio mzima wa kumbukumbu katika ubongo hii hupelekea watu wengi kupata magonjwa kama vile stroke au magonjwa mengine yafananayo na hayo hasa yale yasababishwayo na msawazo mbaya wa homoni mwilini.
Msongo wa mawazo wa mawazo ni jambo la kawaida na ni jambo la kila siku katika maisha ya binadamu.Msongo wa mawazo husababishwa na mambo mabalimbali kama vile;
ü  Matukio makubwa katika maisha kama vile kutalikiwa,kupata mimba isiyotarajiwa,kufeli mitihani,kifo cha Yule tumpendaye sana au mtu wako wa karibu,kufukuzwa kazi n.k
ü  Matukio ya kila siku kama vile changamoto za kazini kwako (biashara,shambani,ulipoajiriwa nk)
ü  Changamoto za kimazingira
ü  Magonjwa
Hayo ni baadhi tu ya mambo yasababishayo Msongo wa mawazo.Ukweli ni kwamba msongo wa mawazi kudhibitiwa ili usifikie kiwango cha kuleta madhara, leo nimechambua baadhi ya mambo ambayo yanaweza kukuwezesha kudhibiti msongo wa mawazo.
1. Weka Malengo yanayotimizika
Binadamu tuna uwezo na sababu tofauti juu ya malengo tunayo jiwekea.Hata uwezo wa kufikia malengo pia hutofautiana  hivyo, unapoweka malengo yako hakikisha unazingatia uwezo wako na muda ulionao ili kuweza kuyafanikisha. Kamwe usiige malengo ya watu wengine bila kupima rasilimali ulizonazo katika kufikia malengo hayo, daima zingatia uwezo wako ili malengo yako yaweze kufanikiwa na kuepuka kupata msongo wa mawazo.
2. Tazama tatizo kama Changamoto wala si kikwazo
Katika maisha huwa tunakutana na mambo ambayo hatukutaka kukutana nayo na pia tunashindwa kupata yale tuliyoyataka, karibu kila mtu huwa anapitia hali hii kwa namna moja au nyingine. Jifunze kukabili matatizo yako kama changamoto na sio kama mlima mkubwa usiopandika. Jaribu kukubali mambo kwa busara zaidi, na utulivu huku ukitafakari nini cha kufanya ili kulipata lile ulilo kusudia. Changamoto iwe ni chachu ya wewe kuzidi kukazana na kujaribu zaidi.
3. Ondoa hofu katika kila jambo unalotaka kulifanya
Hofu na wasiwasi hukupelekea kutokufanya maamuzi sahihi katika muda sahihi hii yaweza kukusababishia msongo wa mawazo. Uwe na ujasiri wa kuamua mara baada ya kutafakari pande zote kwa makini na kuona faida na hasara za kila upande. Usihofu sana juu ya kuweza kufanya makosa hadi ukaishia kupata msongo wa mawazo, mara nyingine watu hujifunza kutokana na makosa.
4. Kutana na wataalam (Wanasaikolojia au washauri nasaha)
Pale unapokutana na jambo ambalo umeshindwa kulitatua ni vyema ukamshirikisha  mtaalam na ikibidi mzazi wako au mlezi, rafiki wa karibu au mume/mke. Jifunze kutokuweka mambo yanayokuumiza moyoni maana katika hali hiyo ni rahisi sana kupata msongo wa mawazo.
5. Kula chakula bora kwa wakati
Mara nyingi tunakuwa na shughuli nyingi kiasi cha kusahau kula ,na hata inapotokea tunakula ni ili kukidhi njaa tu wala si mahitaji halisi ya mwili . Ni muhimu sana mwili wako upate chakula chenye virutubisho bora na pia unakunywa maji ya kutosha.
6. Fanya mazoezi

Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na pata muda wa kutosha wa kupumzika kila siku kila unapojisikia una msongo wa mawazo .
Hayo aliyojadiliwa hapo ni sehemu tu ya utatuzi wa msongo wa mawazo.Watu wengi hutumbukia katika gharama za matibabu na wadawa bila kujua wanatibu nini maana huenda katika hospital mbalimbali napengine huambiwa “HATUONI UGONJWA” kama nawe ni mmoja wao tafadhali wasiliana nasi tutatue shida yako.

0 Maoni:

Post a Comment

Tafuta  hapa

Kuhusu sisi

Karibu kwenye Blog hii, naamini hautatoka bure na wala hautajuta kuitembelea Blog hii. Karibu sana

Habari Maarufu

Blog Malimbali

All rights reserved by Mwafrikasili - Blog design by ARM's pRo. Powered by Blogger.

Tafsiri

Hati Miliki

© 2013 Mwafrikasili


Jiunge Nasi

Jisajilikwenye blog hii
Twitter
Facebook